KVK CHOIR
Kundi hili nimaalumu kwa kazi ya Mungu Aliye hai. Staily ya uimbaji wetu ni vocal na mziki wa slow dance, kucheza kidogo Vocal zaidi ili ujumbe ufike zaidi kwa walengwa. Tunahudumu kwenye Semina, mikutano ya Injili na Ibadani. Tunatangaza Injili ya Kr isto Aliye Hai, karibu uimbe nasi wakati huu tunapo subiri ujio wa Yesu mara ya pili ambao ukaribu sana. Tukaimbe pamoja wimbo mpya wa Musa na Mwanakondoo. Moto wetu: Tufamilia moja. Zaburi 150:1-6 [1]Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. [2]Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. [3]Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; [4]Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; [5]Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. [6]Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.

Comments
Post a Comment